WATU 40 WAMEFARIKI BAADA YA GARI LA MAFUTA KUWAKA MOTO NCHINI KENYA. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

WATU 40 WAMEFARIKI BAADA YA GARI LA MAFUTA KUWAKA MOTO NCHINI KENYA.

Takribani watu 40 wamefariki nchini Kenya kufuatia Lori la kubebea mafuta kulipuka.Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya limetoa taarifa kuwa gari hilo lilikuwa likielekea nchini Uganda lakini lilionekana kumshinda dereva kabla ya kugonga magari mengine na kulipuka eneo la barabara ya Nairobi Naivasha kaskazini Magharibi mwa mji mkuu Nairobi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa mlipuko mkubwa uliotoka katika gari hilo ulilipua nagari mengine na baadhi ya watu waliokuwa wamesimama jirani na barabara.

Miongoni mwa magari yaliyoteketea ni pamoja na daladala 3 yaliyokuwa na abiria 14 ambao wote wamefariki.Baadhi
ya vyombo vya habari nchini Kenya vinataja idadi ya waliofariki ni zaidi ya 40
Miili mingi kwenye ajali hiyo imeungua kiasi cha kushindwa kutambulika.Hali za
Waliojeruhiwa zinaelezwa kuwa ni mbaya sababu ajali hiyo imetokea ikiwa Madaktari wanaingia katika Siku ya tatu ya Mgomo wao. Hizi hapa baadhi ya Picha za Moto huo :
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More