Aliyenajisi Binti wa Miaka 9 Apigwa Mvua Ya Miaka 30. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Aliyenajisi Binti wa Miaka 9 Apigwa Mvua Ya Miaka 30.

Mahakama ya wilaya ya Ilala imemhukumu Shabani Huseni miaka 29 kifungo cha Miaka 30 Jela baada ya kupatikana na Hatia ya kunajisi mtoto wa miaka 9.Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi Catherine Kihoja alisema Upande wa Mashitaka ulipeleka Mashahidi watano ambao wameweza kuthibitisha mashitaka bila kuacha shaka yoyote.


"Kutokana na Ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo umeweza kuthibitisha mashitaka hivyo mshitakiwa ninamtia Hatiani kama alivyoshitakiwa"alisema Hakimu Kioja.Kabla ya kutolewa kwa Adhabu hiyo wakili wa Serikali Neema Moshi aliomba Mahakama kutoa adhabu
Kali kwa Mujibu wa Sharia kwa kuwa Mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho Ameathirika Kisaikolojia na kupata Madhara kiafya.

Aidha mshitakiwa aliiomba Mahakama impunguzie Adhabu kwa kile alichodai kwamba hana ndugu Ombi ambalo lilitupiliwa mbali.

Inadaiwa Mshitakiwa alitenda kosa hilo Julai mwaka Jana Eneo la Kipunguni B Moshi bar wilayani Ilala ambapo alimbaka binti wa Miaka 9.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More