Mtoto wa Rais wa Msumbiji auawa kwa Kupigwa Risasi. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Mtoto wa Rais wa Msumbiji auawa kwa Kupigwa Risasi.

Mtoto wa kike wa Rais wa zamani nchini Msumbiji Armando Guebuza, Valentino Guebuza ameuawa kwa kupigwa risasi siku ya Jumatano katika mji mkuu Maputo.Bi Guebuza aliyekuwa na umri wa miaka 36 imeripotiwa alipigwa risasi mara kadhaa nyumbani kwake na kufariki dunia kutokana na Majeraha wakati akipelekwa Hospitali.


Kufuatia tukio hilo aliyekuwa mume wake Zofino Muiuane amekamatwa katika moja ya Maeneo ya burudani mjini
Maputo.Mwaka 2013 Valentino Guebuza alitajwa na jarida la Forbes la nchini Marekani kuwa mwanamke namba 7 mwenye uwezo barani Afrika akijihusisha zaidi na biashara za Mawasiliano pamoja na biashara nyingine za Familia.

Valentino na mumewe walioana mwaka 2014 ambapo viongozi mbalimbali na wafanyabiashara barani Afrika.
Waliohudhuria harusi  yao ikiwa ni pamoja na Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma, Mfalme wa Swaziland mswati 3 na mwanamke namba moja kwa Utajiri Afrika ambaye ni mtoto wa Angola Isabela Dos Santos.

Rais Armando Guebuza aliachia madaraka mwaka 2014 baada ya kuwa ametumikia nchi hiyo kwa Mihula miwili.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More