Mchezaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania Christian Ronaldo CR 7 anaumaliza mwaka 2016 kwa kufanikiwa kushinda tuzo ya 9 katika Soka kwa mwaka 2016 baada ya kufanikiwa kushinda Tuzo ya Globe Soccer Award akiwa Dubai Tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia wa Globe Soccer Award 2016.
Katika Tuzo hiyo ya Globe Soccer Award 2016 Ronaldo alikuwa anawania na Lionel Messi, Jamie Vardy, Gonzalo Higuan na Antoine Griezman.Hii ni Mara ya 4 Ronaldo anashinda tuzo hiyo aliwahi kushinda mwaka 2011, 2013 na 2014.
Ronaldo nwaka huu 2016 ameshinda Tuzo ya Mchezaji bora wa Ulaya, The World Soccer, Four Four Two, Espy, Di Stefano Award, Goal.Com Award, Fifa Club Golden Ball na Balloon D'OR.
Hata hivyo hivi karibuni pia Ronaldo alitangazwa kuwa Mwanamichezo bora wa mwaka Ulaya 2016 tuzo iliyoandaliwa
Na vyombo vya Habari 27 barani Ulaya.
Ronaldo ndiye mchezaji wa kwanza wa Soka kuwahi kushinda tuzo hiyo.