Msanii mkongwe wa Muziki Lucas Mkenda au Mr Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mitandao ya Kijamii.Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa Nchini Tanzania.
Mr Nice ambaye yupo Nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigia simu kwa wingi na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuwa kuna Mtandao umeandika Taarifa za Uongo kwamba Amefariki.Kupitia Mtandao wa Facebook Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii.
"East Afrika Vibes nawashukuru sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu, Ila mungu atawalipa kadri ya vile Mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia Leo......Mungu ni wetu sote na Hasikilizi amri za Binadamu so atakapohitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie East Afrika mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua.....Kama nyie hamuoni Thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko ni kama Lulu na Maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa......Hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo.......Im Total dissapointed kwa kweli.....Mungu awape Stahiki yenu....Thanks sana Eatv 13.12.2016.