Saida Kalori Ambariki Darasa kwa Muziki Amlaumu Mtayarishaji. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Saida Kalori Ambariki Darasa kwa Muziki Amlaumu Mtayarishaji.

Mwimbaji wa muziki wa Asili Saida Kalori ambaye wimbo wake "Maria Salome" umepata mashavu mawili makubwa mwaka huu kwa wakali wa Bongo flava Diamond na Darasa amezungumzia kitendo cha Darasa kuweka vionjo vya wimbo wake huo mpya bila kuomba ridhaa yake.

Darasa aliachia wimbo ambao sasa "watoto wa mjini" wanauita "Wimbo wa Taifa wa Bongo Flava" alioubatiza jina la MUZIKI ukiwa na vionjo vya "Maria Salome siku chache baada ya Diamond kuachia Salome yenye vionjo hivyo ambavyo yeye aliomba ridhaa kwa Uongozi wa Saida".
Akizungumzia uamuzi huo wa Darasa, Saida Kalori amesema kuwa hana tatizo naye kwa kuwa kufanya hivyo amekuza muziki, lakini alitupa lawama kwa Mtayarishaji wa wimbo huo kutoomba ridhaa ya kutumia vionjo hivyo.

Namnukuu "Siwezi kumfanyia chochote Darasa kwa kuwa hii ni njia ya muziki wetu kukua, unaweza kuonekana una roho mbaya ukikataza watu wasitumie kazi zako ila kufuata taratibu ni vizuri zaidi" alimalizia Saida Kalori.
Hivi karibuni Rapa Darasa alisema kuwa alipanga kumshirikisha Saida Kalori kwenye wimbo huo kuweka vionjo lakini aliahirisha baada ya Diamond kuachia Salome kabla yake.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More