Ahukumiwa Miaka 25 Jela Au Faini Ya Bilioni 3.7 Kwa Kujihusisha na Biashara Ya Meno Ya Tembo. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Ahukumiwa Miaka 25 Jela Au Faini Ya Bilioni 3.7 Kwa Kujihusisha na Biashara Ya Meno Ya Tembo.

Mahakama ya Hakimu mkazi Tanga imemtia hatiani na kumuhukumu kwenda Jela miaka 25 au kulipa Faini ya sh bilioni 3.7 Mfanyabiashara Charles Kijangwa kwa kujihusisha na biashara ya Meno ya tembo.Mshitakiwa huyo alikabidhiwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa na Askari wa kikosi cha kuzuia Ujangili kanda ya Mashariki na Pwani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wilaya ya Lushoto.


Hakimu mkazi Cresian Kisongo ametoa hukumu hiyo kwa Kijangwa ambayo aliruka dhamana tangu mwaka 2010 takribani miaka 6 sasa.Wakili wa Serikali
Mwandamizi Saraji Iboru alidai mahakamani kuwa mshitakiwa Kijangwa
alikuwa akitafutwa na Serikali kwa muda mrefu tangu mwaka 2010 ambapo aliruka dhamana katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 6 ya mwaka 2007 iliyokuwa ikimkabili yeye pamoja na wenzake Michael Msuya na Nyaisa Makori.

Mshitakiwa Kijangwa alitenda kosa hilo November 2005 na April 2006 kwa kusafirisha Makontena mawili ya Tembo yenye Ujazo wa Tani 5000 yaliyokamatwa katika bandari ya Konshug nchini Taiwan.

Makontena hayo ambayo yalitokea katika bandari ya Tanga yakiwa na Shehena ya Kamba za Katani na Meno ya Tembo ndani yake yalikuwa yanapelekwa Manila nchini Philippine.



SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More