Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro.

Msemaji wa klabu ya Simba SC Haji Manara ameiomba TFF kumtoa kifungoni Msemaji wa watani wao wa jadi Yanga SC Jerry Muro.Muro alipigwa Pingu ya mwaka mmoja kutoshiriki soka na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 3.


Manara amekutwa na Upweke wa kiushindani katika tasnia yake na ameamua kutumia mtandao wa Instagram kumuomba Rais wa TFF Jamal Malinzi kumfikiria na kumsamehe mtani huyo ili waendelee kubadilishana tambo,Majigambo na Uzoefu hivyo ndivyo alivyoandika kwenye Instagram :

"Kwako Rais wa TFF,kwanza nikutakie heri na baraka katika sikukuu hii kubwa kabisa duniani kote, nnakuandikia Ujumbe huu mfupi na wa wazi kwako, nikiamini wewe ni MTU mwelewa na mwenye huruma na Upendo pia kiongozi
Mwenye maoni ya dhati kwa Maendeleo ya Soka nchini, kwa vigezo hivyo na ukizingatia Leo tupo katika sherehe ya Noeli atalikubali ombi langu binafsi nitakalokuomba.Nimekaa nimetafakari sana nimeamua kumuombea Msamaha mtani wangu Jerry Muro ambae TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa Miguu nnafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake",

"Nnajua kwa kufanya hivyo atakuwa kashajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa Fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa Ujumla.
Ninafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili Mimi binafsi lakini Yale yasahapita na binafsi amenihakikishia kutorudia tena na ninaamini viongozi na Mashabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema ambayo inathibitisha Uungwana tulio nao wanasimba.Tunamiss rikaka zake,zinazoongeza Ushabiki na Utani wetu wa Jadi, Kwangu Mh Rais nina hakika utatumia mamlaka yako kumfungulia mtani wangu Jerry na kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia Huru".

"Ukizingatia Jerry sio mzoefu sana wa Utamaduni wa siasa za Mchezo huu murua zaidi duniani.Mwisho nikutakie mapumziko mema ya kuelekea mwishoni mwa mwaka wako.
Haji Manara.
























SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More