Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF limetangaza majina ya wachezaji watatu watakawania Tuzo ya Mchezaji Bora Afrika Mwaka huu.
Wachezaji waliotajwa kwenye majina hayo ni pamoja na Pierre_Emerick Aubameyang wa Gabon na klabu ya Borussia Dortmund.
Wengine ni Riyad Mahrez wa Algeria na Leicester City pamoja na Sadio Mane wa Senegal na klabu ya Liverpool.
Wachezaji wengine waliotajwa kuwania
tuzo ya Mchezaji bora wanaocheza ligi za ndani ni Pamoja na Golikipa wa Uganda Dennis Onyango na Khama Billiat wa Zimbabwe wote wanachezea klabu ya Mamelodi Sundowns na Rainford kalaba kutoka Zambia.
Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Januari 5 mwakani jijini Abuja Nigeria.