Sirro asema atatoa taarifa juu ya Boss wa Mtandao wa Jamii Forum kukamatwa. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Sirro asema atatoa taarifa juu ya Boss wa Mtandao wa Jamii Forum kukamatwa.

Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media kampuni inayomiliki mtandao maarufu Jamii Forum Maxence Melo anashikiliwa na Polisi.Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao huo Max amekosa dhamana.Taarifa kutoka Jeshi la Polisi linadai kuwa Melo amekataa kuonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo ambapo walikuwa wakihitaji majina ya baadhi ya watumiaji wa mtandao huo."Huku kiongozi huyo alikataa kutoa taarifa hizo kwa kile alichoeleza kuwa kufanya hivyo ni uvunjwaji wa Sheria na Haki za Wananchi".


Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es salaam Simon sirro amesema kuwa tuhuma za kukamatwa kwa Mkurugenzi wa Jamii Forum na Kushikiliwa na Jeshi la Polisi atazitolea ufafanuzi Ijumaa ya wiki hii.

Aidha Kamanda Sirro amewatoa hofu waandishi wa Habari kuhusu kauli ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi GRC
Ubungo kibangu Antony Lusekelo kuwa waandishi waliomwandika vibaya watakufa.Kamanda Sirro amesema kauli hiyo inaweza kumpa hofu Mpagani pekee.

Namnukuu "kwa hiyo mpagani akisikia ya mtu mwingine Mpagani kwa sababu anafikiria Upagani wake ataanza kuwa na wasiwasi lakini kwa sababu unajua mungu ni huyo mmoja na yeye ndiye aliyekuleta duniani pia ndiyo atakayekutoa duniani hupaswi kuwa na hofu"alimalizia Kamanda Sirro.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More