Bodi ya mikopo ya Wanafunzi wa elimu ya juu HESLB Jana ilichapisha hadharani majina ya wadaiwa sugu walionufaika na mikopo wakiwa vyuoni lakini hadi sasa hawajarejesha mikopo hiyo.Majina hayo yameanza kwa wanafunzi waliomaliza chuo mwaka 1994/1995
huku majina ya watu maarufu na watoto wa vigogo wenye uwezo mkubwa wa kifedha nayo yakiwemo miongoni mwa wadaiwa sugu.
Miongoni mwa majina ya watu maarufu waliokuwa katika Orodha hiyo iliyochapishwa ni pamoja na Katibu Mkuu wa shirikisho la soka Tanzania TFF Mwesigwa Selestine ,aliyekuwa katibu mkuu TFF Frederick Mwakalebela
Mkurugenzi wa Itifaki Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo John Mrema Meya wa Ubungo Chadema Boniface Jacob.
Jerry Muro ambaye ni afisa habari wa Yanga naye yumo katika Orodha hiyo
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Uhamishaji mamlaka ya Usimamizi wa Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii SSRA Sarah kibonde na Mwanasheria maarufu Majura Magafu.Pia mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Adda E Lowassa nayo ni miongoni mwa wadaiwa sugu waliotajwa.Aidha kuna baadhi ya majina ambayo yamedaiwa ni ya watoto wa vigogo lakini haijathibitisha kama ni watoto wao au majina yamefanana.
Miongoni mwa majina hayo Lowassa Godson Ngoyai ambaye anadaiwa kuwa ni mtoto wa Lowassa na Pombe Ruth John ambaye anadaiwa kuwa ni mtoto wa Rais Dk John Pombe Magufuli.Bodi ya Mikopo ya Elimu ya huu ilitangaza kuwa inatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu wote kurejesha mikopo kinyume na hapo
watafikishwa mahakamani.Aidha mbali na kufikishwa Mahakamani wadaiwa sugu wote watatakiwa kulipa gharama zilizotumiwa na Mamlaka hiyo kuwatafuta.