Kufuatia kiwango kizuri alichokionesha Henrikh Mkihitaryan kwenye mchezo dhidi ya Zorya Luhansk kimezua mjadala mkubwa mitandaoni huku watu wakijiuliza kocha Jose Mourinho alimuacha benchi kwa muda mrefu ili ajirekebishe baadhi ya mapungufu na kumwongezea hasira zaidi ya kupigania namba katika timu yake ya Manchester United.
Mkihitarayan aliibuka mwezi uliopita akitokea benchi na kufanya makubwa uwanjani.Amekuwa akifanya vizuri kila anapoingia uwanjani na kupelekea kuanzishwa kwenye game ya Europa League dhidi ya Zorya Luhansk.
Mkihitarayan aliifungia Manchester United goli kwenye ushindi wa magoli 2_0 dhidi ya Zorya Luhansk dk 48 na Zlatan Ibrahimovic aliyefunga goli la pili dk 88.
Lilikuwa bonge la bao baada ya kuchukua mpira akiwa nusu ya Uwanja upande wa Manchester United kisha kuwapunguza wachezaji kadhaa na kufunga goli.Lilikuwa goli zuri kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 na huenda ataendelea kulikumbuka kwa miaka kadhaa ijayo.Manchester United wamemaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi A wakiwa wamefanikiwa kufuzu katika hatua inayofuata.
Haya hapa matokeo ya mechi zote zilizochezwa usiku wa Alhamisi Disemba 8 nimekusogezea hapa :