Msichana Redna Raphael mwenye umri wa miaka 19 amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka Ghorofa ya Saba katika Jengo la Harbour View Tower maarufu kama J.M Mail lililopo katika makutano ya mtaa wa Samora na barabara ya Morogoro jijini Dar es salaam.
Redna ambaye ni Mfanyakazi wa kampuni ya Usangu Logistics ltd yenye ofisi zake ndani ya jengo hilo inadaiwa "alichukua uamuzi huo muda mfupi baada ya kuzungumza na simu na mtu ambaye bado hajafahamika wanahusiana vipi".
Hata hivyo binti huyo alinusurika baada ya kuangukia kwenye moja ya Mabomba
yanayotoa moshi kwenye Jenereta ya Jengo hilo lillilopo Ghorofa ya kwanza ambako walinzi wa Jengo hilo walimuokoa.
Meneja wa Kampuni hiyo ya Usangu Mazar Dadkarim alisema wakati tukio hilo linatokea hakuwepo Ofisini bali alipatiwa taarifa na Wafanyakazi wenzake waliokuwa ofisini.