Wajumbe wathibitisha Ushindi wa Donald Trump. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Wajumbe wathibitisha Ushindi wa Donald Trump.

Baada ya kuwepo taarifa za kwamba huenda Ushindi wa Rais Mteule wa Marekani Donald Trump ungetenguliwa hatimaye Wajumbe wa Baraza la Uchaguzi la Marekani (Electoral College) limepiga kura na kutoa tamko rasmi kuwa Ushindi wa Mwanachama huyo wa Republican ni halali.


Donald Trump atakayekuwa na makamu wake Mike Pence wameidhinishwa na Baraza hilo kwa ushindi wa kura zaidi ya 270 ikiwa ni wiki 6 baada ya kupita Uchaguzi Mkuu uliofanyika Nchini humo Nov 8 2016.Japokuwa kwenye Upande wa kura za Wananchi wa kawaida bado Hilary Clinton ameendelea kuongoza kura zaidi ya Milioni 3 baada ya Matokeo kutangazwa.

Kupitia kurasa zao za Twitter Donald Trump na Makamu wake Mike Pence wameonesha furaha yao baada ya kuthibitishwa kwa ushindi wao na kuwa Rais wa 45 wa Marekani.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More