Ajali mbaya imetokea jana jioni eneo la Ifunda Iringa imeua watu 9 na wengine 18 kujeruhiwa Ajali hiyo imehusisha lori la mizigo kugonga gari dogo la Abiria Hiace.Kamanda wa Polisi wa Mkoa Amina Masenza
alisema dereva wa lori lililotokea Mbeya kwenda Dar es salaam alishindwa kufunga breki ya gari hilo na kugonga Hiace hiyo iliyoogeshwa pembezoni mwa barabara.
"Lori limeharibika kabisa na Hiace pia imeharibika,Lori hilo liliposhindwa kufunga breki liligonga Hiace hiyo ambayo ilikuwa na abiria na kwenda mbele kugonga watembea kwa miguu" alisema kamanda.Madereva wa magari hayo wote wamejuruhiwa na wamelazwa hospital ya mkoa wa Iringa na majeruhi wote.
"Dereva mmoja yupo chumba cha upasuaji kwa kuwa mguu wake umevunjika na mwingine yupo wodini".Kamanda wa Polisi ametoa tahadhari kwa madereva ambao magari yao mabovu kuhakikisha wanayatengeneza kwanza kabla ya kuyaingiza barabarani kwani yanahatarisha maisha ya watu wengi.Hizi hapa ni picha za Ajali hiyo: