MCHEZAJI WA MBAO FC AFARIKI BAADA YA KUGONGANA NA MCHEZAJI WA MWADUI FC. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

MCHEZAJI WA MBAO FC AFARIKI BAADA YA KUGONGANA NA MCHEZAJI WA MWADUI FC.

.Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Mbao Fc under 20 Ismail Mrisho Khalfan anayevalia jezi nambari 4 amefariki dunia baada ya kuanguka uwanjani Kaitaba wakati wa mtanange wao dhidi ya timu ya vijana ya Mwadui Fc ikiwa ni mechi ya mwisho ya kumaliza duru la kwanza la  ligi ya vijana.

Ismail khalfan amefariki mara baada ya kufikishwa Hospital ya serikali ya mjini Bukoba.Ismail Khalfan kabla ya kufikwa na umauti aliweza kuifungia timu yake bao la kwanza na la pili lilifungwa kwa mkwaju wa penati hivyo mtanange kumalizika kwa 2_0

Kabla ya kuanguka Ismail aligongana na beki wa Mwadui Fc na baadaye akiwa peke yake alianguka chini lakini aliinuka halafu
akaanguka tena na kutokana na ukosefu wa huduma ya kwanza na gari la wagonjwa katika uwanja wa Kaitaba kulipelekea marehemu kupandishwa gari la zimamoto na kupelekwa Hospital ambapo mauti yalimkuta mchezaji huyo.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More