Balozi wa Urusi nchini Uturuki Andrei
Karlov ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa Jumatatu na Afisa wa Polisi wakati akihutubia kwenye Maonesho ya Picha mjini Ankara kama kisasi kutokana na ugomvi wa Syria.
Balozi huyo mwenye umri wa miaka 62 alipigwa risasi kadhaa na Mtu huyo aliyekuwa amesimama nyuma yake huku
Akipiga kelele "Allahu Akbar, allahu Akbar,We die in Allepo,you die here"alisikika akisema Pia "Only death will take me out of here".
Muuaji huyo aliyekuwa amevaa suti na tai amejulikana kwa jina la Mevlur Mert Altintas mwenye miaka 22,Inadaiwa alianza kupiga risasi kwanza hewani kabla ya kumlenga balozi huyo.Baada ya hapo aliwageukia wote wengine waliokuwa hapo na kuwajeruhi watu kabla ya naye kuuawa na Polisi.
Mauaji hayo yamekuja baada ya siku kadhaa za maandamano nchini Uturuki dhidi ya namba ya Urusi inayohusika nchini Syria.Tayari Rais wa Urusi Vladimir Putin amelaani vikali tukio hilo. Hizi hapa Picha za Tukio hilo :