Taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania kuhusu uzushi dhidi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo ( WAMA ) | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania kuhusu uzushi dhidi ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo ( WAMA )

Imetoka taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania kuhusu siku za hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii imechapisha taarifa zinazomhusisha mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mama Salma Kikwete na taasisi anayoiongoza ya wanawake na maendeleo WAMA kwamba imeshindwa kulipia kodi mizigo mikubwa iliyoingiza nchini na hivyo kuwa hatarini kupigwa mnada.

Taarifa hizi zimemhusisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt John Pombe Magufuli kuwa anahusika kuzuia mizigo hiyo bandarini mpaka
hapo itakapolipiwa kodi.Rais Magufuli amesikitishwa sana na Uzushi huo unaofanywa kwa lengo la kumchafua Rais wa awamu ya 4 Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na familia yake.Amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuacha kuandika na kuchapisha taarifa za uzushi na badala yake vizingatie weledi na kufuata sheria.

"Nimesikitishwa sana na uzushi unaofanywa dhidi ya Rais Mstaafu na Mke wake,tafadhali wale mnaotengeneza uzushi huu acheni Mara moja na muacheni Rais mstaafu apumzike".Rais mstaafu amefanya kazi kubwa ya kulitumikia Taifa hili,amestaafu anapumzika,
narudia muacheni apumzike,serikali haitaendelea kuvumilia uzushi na uchonganishi huu unaofanywa kwa makusudi ili kuwachafua viongozi wastaafu".Ameonya Rais Magufuli.

Imetolewa na  Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais,
IKULU  Dar es salaam.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More