Kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo katika ofisi ndogo za Chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam kujadili masuala mbalimbali ya chama hicho.
Baada ya kikao hicho kufanyika katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho Nape Nnauye alizungumza na waandishi
wa habari waliokuwepo katika Ofisi hizo kuhusu masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye kikao hicho.Nape Nnauye alisema kuwa ajenda kubwa iliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuhusu tathimini ya Chama hicho iliyofanywa kwa takribani mwaka 1 baada ya kumalizika kwa Uchaguzi mkuu wa mwaka Jana.
Tathimini hiyo ameeleza kuwa imeanzia ngazi ya Shina ya chama ikihusisha wanachama wakitoa maoni yao juu ya mwenendo wa chama katika kipindi cha uchaguzi.Mbali na hilo kikao hicho cha CCM kimefanya teuzi mbalimbali kujaza nafasi zilizokuwa wazi ndani ya Chama.
Miongoni mwa walioteuliwa ni pamoja na Makongoro Nyerere ambayo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara.Aliyekuwa Mbunge wa Bunda Steven Wassira ameteuliwa kuwa msemaji wa CCM akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Christopher OleSendeka.Wakati huo huo Peter Maduki ameteuliwa kuwa Mweka Hazina
Wa CCM akichukua nafasi ya Zakia Meghi.