Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba amesema kuwa huenda watu waliokutwa wamekufa na kutupwa kwenye Mto Ruvu kwa kufungwa kwenye viroba walikuwa ni wahamiaji haramu ambao walikumbwa na mkasa huo toka kwa wasafirishaji wa Wahamiaji hao.
Akizungumzia tukio hilo mkoani Singida waziri Mwigulu amesema kitendo cha kukutwa kwa wahamiaji zaidi ya 80 wakiwa na majeraha na hawajiwezi mkoani Pwani kinahusisha kwa namna moja au nyingine maiti zilizookotwa Mto Ruvu.
Waziri Mwigulu amesema kuwa watu hao ambao wamezikwa na Serikali licha ya ndugu au Taifa lolote kujitokeza Sheria inawaruhusu kufanya hivyo kutokana na kutokutambulika kwa watu hao.
Waziri Mwigulu amesema bado wanaendelea na Uchunguzi juu ya Matukio hayo ikiwa na Operesheni mbalimbali za kutokomeza Matukio ya Kihalifu pamoja na Wahamiaji haramu Nchini.