Kiungo wa klabu ya Chelsea Oscar Dos Santos anatarajiwa kuwa Mchezaji atakayekuwa analipwa Mshahara Mkubwa zaidi duniani na kuwafunika Ronaldo na Messi.
Imedaiwa kuwa klabu inayoshiriki ligi kuu ya China Shanghai SIPG imeshaanza kukamilisha mipango yao ya kumsajili Mchezaji huyu mwezi Januari kwenye dirisha dogo la
Usajili ambayo itaigharimu timu hiyo kiasi cha Paundi Milioni 60 kama fedha ya Usajili.
Oscar anatarajiwa kulipwa Mshahara wa
Paundi laki nne kwa wiki na kumfanya awe Mchezaji anayelipwa zaidi duniani.
Kwa sasa Ronaldo na Messi ndio wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa zaidi duniani wote wakipokea kiasi cha Paundi 365,000 kwa wiki.