Mwaka 2016 unaondoka na ndoa nyingine iliyoonekana imara kwa macho ya wengi.Ndoa ya T.I na mkewe Tiny imefikia ukingoni baada ya kudumu kwenye ndoa kwa muda wa miaka 6.Tiny muimbaji wa zamani wa kundi la Xscape ameomba talaka kutoka kwa mume wake mwezi huu.
Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ uhusiano wao uliingia doa zaidi baada ya kusambaa mtandaoni Picha za Tiny akicheza mziki na Floyd Mayweather adui mkubwa wa T.I kwenye Party ya Halloween ya Mariah Carey.
Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2010
na pamoja wana watoto 3 King, Major na
wa kike Heiress Harris aliyezaliwa March
Licha ya kuachana habari zinadai kuwa wataendelea kuwa marafiki kwa ajili ya watoto na familia yao.