Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo ambaye amekuwa akizuiliwa na maafisa wa Polisi tangu Jumannne amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam na kushitakiwa kwa makosa matatu.
Makosa hayo ni kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa Nchini na kuzuia Uchunguzi wa Polisi kwa mujibu wa Sharia ya makosa kimtandao.
Melo anadaiwa kusimamia Anwani ya Mtandao ambayo haijasajiliwa nchini Tanzania kinyume na kifungu 79(c) cha Sheria za Mawasiliano ya Elektroniko na Post ya mwaka 2010.
Pamoja na kanuni za Mtandaoni nambari
428 za mwaka 2011. Nyaraka za Mashitaka zinasema anwani ya Mtandao
ya Jamiiforums.com ambayo haijasajiliwa chini ya kikoa cha Anwani za Tanzania cha .tz.
Kwenye kosa jingine ameshitakiwa kuzuia Uchunguzi kinyume na kifungu cha 22(2) cha sheria za Uhalifu wa kimtandao ya mwaka 2015.
Nyaraka za mahakama zinasema "akiwa anafahamu kwamba jeshi la Polisi lilikuwa linafanya Uchunguzi wa Jinai kuhusu Mawasiliano za kielektroniki kwenye Mtandao wake akiwa na nia ya Kuzuia Uchunguzi alikataa kutii agizo la kufichua maelezo aliyo nayo.kwa mujibu wa Taarifa zilizokuwa zimetolewa na Jamii Forums jana walisema kuwa "SERVER" ya tovuti yao hapo Nchini Tanzania wala barani Afrika lakini hawakutaja ni nchi gani Ilipo.
Melo amepelekwa rumande Keko hadi Jumatatu Disemba 19 mwaka huu baada ya kukosa mdhamini katika shitaka la tatu la kumiliki na kuendesha tovuti ambayo haijasajiliwa Nchini.