Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia mchimba dhahabu Shija Salum 38 mkazi wa Kahama Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua rafiki yake na kula ubongo wake.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari aliwambia waandishi wa habari kwamba pamoja na mtuhumiwa kula ubongo wa rafiki yake aliyetambuliwa kwa jina la Shija pia alitafuna sehemu zake za siri baada ya kuzikata.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari tukio hilo lilitokea disemba 25 mwaka huu usiku katika kijiji cha Manyanya kata ya Makongoros wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. "Alisema mtuhumiwa na marehemu walifika kijijini hapo wakitokea Shinyanga miezi 3 iliyopita,inasemekana wawili hao walikuwa marafiki kwani walifika wilayani Chunya kwenye Machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na Mfanyabiashara Teddy mwantega".
"Siku ya tukio hilo marehemu Shija alikuwa amejilaza mahali na hapo ndipo alipofika rafiki yake huyo akiwa na Panga mkononi na kumkata kwa nguvu kichwani.Baada ya hapo alimvua nguo na kuzikata sehemu za siri za marehemu na kuzishika mkononi.Wakati akiwa na sehemu hizo za Siri mkononi alichukua Ubongo wa Marehemu na kuula kisha akatafuna zile sehemu za siri za marehemu"alisema Kamanda.
Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika alisema Kamanda Kidavashari.