Bingwa wa Dunia wa ngumi za kulipwa mwenye rekodi ya kutopeza kirahisi mechi zake katika Tanzania anayekipiga uzito wa kati Francis Cheka ametangaza rasmi kuachana na Mchezo huo wa ngumi na kujielekeza kwenye Masuala ya kibiashara.
Cheka "NGUMI JIWE" mwana wa Morogoro amesema haya wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro kuhusu taarifa zilizolipotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzagaa kwenye Mitandao ya kijamii vikimhusisha na Utapeli wa kukimbia Ulingoni Disemba 25 mwaka huu jijini Dar es salaam.
Alikotakiwa kupigana na Bondia Dula Mbabe ambapo amebainisha kutofika Ulingoni siku hiyo hakukumaanisha kuhofia Pambano hilo bali ni kutokana na Promota wake Kaike Selagi kutomlipa Fedha zake zote kama walivyokubaliana ambapo amedai alipaswa kulipwa Milioni 9 lakini hadi wanamaliza kupima Uzito alikuwa amepewa milioni 3 pekee.
Akizungumzia azma ya kuachana na Ngumi Cheka amesema kwa muda mrefu amekuwa akipigana bila Mafanikio kutokana na Kudhulumiwa na Waandaaji kulipwa Tofauti na Makubaliano sambamba na Misukosuko ya Hapa na Pale anayofanyiwa na Wapinzani wake na kwamba anaamini wapo baadhi ya watu waliolenga kumshusha kwenye Ngumi badala ya Kumtengeneza Bondia mwingine mwenye uwezo wa kumpiga.
Amesema kwamba kwa sasa atajielekeza kufanya biashara zake na kuahidi ushirikiano kwenye Mchezo wa Ngumi ili kukuza na Kuendeleza Mchezo huo.