Mahakama kuu ya Wilaya ya Serengeti imewahukumu watu 3 kifungo cha miaka 73 jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuingia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na kuua Tembo.Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi Mfawidhi Emmanuel Ngaile wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti.
Amesema adhabu hiyo imetolewa kutokana na Kuridhishwa na Ushahidi uliotolewa na Upande wa Mashitaka.
Waliohukumiwa kutumia adhabu hiyo ya Jela ni Augen Nicodemus, Mwita Marwa na Amos Alexander wote wakazi wa wilaya ya Serengeti.
Aidha Hakimu Ngaile amesema kuwa katika kosa la kwanza la kuingia na silaha ndani ya Hifadhi kinyume cha Sheria za Nchi kwa ajili ya kufanya vitendo vya Ujangili mahakama imewahukunu watumikie adhabu ya miaka 15 jela kila mmoja.
Ngaile ameongeza kuwa kosa la pili ni la kusafirisha silaha kutoka Burundi hadi Tanzania kinyume cha kifungo nambari 18 cha sharia ya Mlipuko ya mwaka 2002 ambapo walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Katika kosa la tatu kupatikana na silaha ndani ya Hifadhi ya Taifa za Serengeti kinyume cha Sharia ya Hifadhi ya Taifa ya mwaka 2002 watatumikia kifungo cha miaka 2 kila mmoja.
Ameongeza kuwa kosa la nne kuingia kwenye Hifadhi bila kibali washitakiwa watatumikia kifungo cha mwaka 1 kila mmoja.
Na kosa la tano la kuua tembo ndani ya Hifadhi adhabu yake ni miaka 10.
Hata hivyo amesema kosa la sita la kupatikana na Nyaraka za Serikali kinyume cha Sheria ya Wanyama Pori namba tano ya mwaka 2009 Washitakiwa wamehukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela kila mmoja.