Msanii bora wa kike Lady Jaydee ameitaja TALAKA yake kutoka kwa aliyekuwa mume wake Gadner G Habash ni miongoni mwa mambo 4 anayoshukuru zaidi kwa mwaka 2016.
Kupitia Mtandao wake wa Instagram Jidee ameposti vyeti vyake vya Ndoa.
Na kuandika "Funga mwaka katika vikubwa ninavyoshukuru 2016 ni kutoka cheti cha Juu na kuingia cheti cha Chini.....Bila kujali wanafikiria nini...Nilifanya hivyo kwa manufaa na furaha yangu, maisha yangu na familia yangu.Namshukuru mungu kwa kunipa nguvu kwao haikuwa kazi rahisi ukizingatia swala la kuogopa watu watakujudge vipi.Baada ya Battle ya nafasi takribani miaka 2....Naomba makofi tafadhali....Sitegemei tena kauli za nilikufanyaje sijui miaka kadha, au emoji zisizoeleweka.Utoto huooo....Mtu akimove on hana haja kufanya utoto wote huo,uki move on hujali chochote.Kwa neema ya Mungu nawaombea wote ambao hamja get over situations mbarikiwe mtoke kwenye kuwaza Past,Maisha mbona ni matamu tu ukiamua
#Kataakuwamtumwa
#Chaguakuwanafuraha
#Gutsoverfear
#Komando
#MoveonNigga.