Rapper Darassa ameendelea kuweka rekodi mpya katika muziki kupitia video yake ya wimbo "Muziki" ikiwa ni siku 28 toka iwekwe kwenye Mtandao wa You tube.Wiki hii video ya wimbo huo imefikisha zaidi ya Views Milioni 2,039,741 ndani ya siku 28.
Ni nadra sana kwa Msanii anayerap kufikisha idadi hiyo ya Views katika kipindi kifupi kama hicho.Wimbo huo wa Muziki umemfanya Darassa kuwa juu zaidi katika muziki kwa wakati huu kutokana na wimbo huo kupigwa kila kona ya Tanzania.
Tayari watoto wa Mjini wanauita wimbo huo wa "MUZIKI" kuwa ni wimbo mpya wa Taifa.Wimbo huo umemfanya Darassa awe miongoni mwa Wasanii wanaotafutwa sana kwa Show wakati huu.