Kufuatia kifo cha mchezaji wa Mbao Fc ripoti iliyotolewa na Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dk Thoma Rutta na kusomwa na kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera Augustine Ollomi inaeleza kuwa kusimama ghafla kwa moyo ndio chanzo cha kifo cha chipukizi huyo wa Mbao Fc ya mwanza Ismail
Khalfan Mrisho.
Taarifa hiyo ilitolewa jana na kamanda huyo alipokuwa akizungumza chanzo cha kifo cha mchezaji huyo kilichotokea Jumapili
wakati wa mchezo wa Mbao Fc dhidi ya Mwadui Fc ikiwa ni ligi ya vijana katika uwanja wa kaitaba mkoani Kagera.Daktari ametoa taarifa ya Uchunguzi na kusema chanzo ni kusimama kwa moyo ghafla.
Marehemu hakuwa na jeraha lolote alisema kamanda Ollomi.Ismail alifikwa na mauti muda mfupi baada ya kugongana na mchezaji wa mwadui alipojaribu kusimama baada ya hapo alianguka tena ndipo alipokimbizwa hospitali mjini Bukoba lakini akafariki.Kabla ya kukumbwa na mauti aliifungia timu yake ya mbao goli la kuongoza ambapo mchezo ulimalizika kwa mbao kupata ushindi wa 2_0.
Ismail alikuwa amepata ufadhili wa kwenda kusoma chuo kikuu cha Louisiana State nchini Marekani kuanzia mwakani.