Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza Pambano lake Nchini India alipopigana na Raia wa Nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa Mpinzani wake huyo hakumpiga ila alibebwa na Mwamuzi.
Akiongea kutoka India Cheka amesema katika raundi ya 3 alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda Meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na Kikohozi na wakati anakifanyia Marekebisho ndipo Mwamuzi akatangaza Mshindi bila ya kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.
"Tatizo nilikuwa nakohoa, nilijiandaa kumpiga yule Vijender"alisema Cheka.
Pia katika mtandao wake wa Instagram bondia huyo aliandika hivi :
"Pale ambapo Matokeo yamepangwa, tunaenda kukamilisha ratiba tu. Refa unaona Mouth Guard imetoka na Unaendelea kuchezesha........WaTanzania nadhani mmeona, tusiwage wanyonge kwao na kwetu pia.....nadhani nimeliwakilisha Taifa vyema, kuitangaza Morogoro,Tanzania, Kiswahili na Kimakonde Pia" alimalizia Bondia huyo.