Watoto wawili wenye umri wa miaka 3 na mwingine 6 wa kijiji cha Patane kata ya Mambamiamba wilayani Same wameuawa kwa kuchinjwa na Panga na baba yao Mzazi Yohana Greson 26 na yeye mwenyewe kujining'iniza kwenye Paa la nyumba.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro
Wilbroad Mutafungwa alisema tukio hill
lilitokea disemba 13 mwaka huu majira ya saa 5 asubuhi katika kijiji cha Patane.
Kamanda alisema Baba huyo alifanya tukio hilo la kutisha baada ya mkewe Eva
Tumaini 29 mkazi wa kijiji cha Ghona kwenda Shambani na kumwacha mumewe nyumbani akiwa na watoto 2 Esta Yohana na Tumaini Yohana.
Ambapo alichukua Panga na kuwachinja
na yeye kujinyonga kwa Kamba kwenye Paa la Nyumba.Kamanda alisema Polisi
Inaendelea na Uchunguzi wa tukio hilo na kwamba Uchunguzi wa awali umebaini Marehemu huyo alikuwa na tatizo la Kifafa.
Alisema miili ya Marehemu wote imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Same kwa ajili ya Uchunguzi zaidi na kwamba Marehemu hakuacha Ujumbe wowote na Uchunguzi ukikamilika ndugu za Marehemu watakabidhiwa miili hiyo kwa ajili ya Mazishi.