Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya Taifa ya Ureno Christian Ronaldo amemshinda hasimu wake wa karibu Lionel Messi na kutwaa tuzo ya Ballon D'or kwa Mara 4.Christian Ronaldo aliisaidia klabu yake ya Real Madrid kombe la klabu bingwa Ulaya huku akiifungia timu yake ya Taifa magoli 3 na kuiwezesha kutwaa kombe la Ulaya Euro 2016.
Mataji mengine ya Ballon D'OR alishinda mwaka 2008, 2013 na 2014.Kwa sasa Ronaldo amepitwa na Messi kwa tuzo 1 ambaye amechukua tuzo hiyo Mara 5 mwaka 2009, 2010,2011, 2012 na 2015.
Tuzo ya Ballon D'OR hupewa Mchezaji bora wa Ulaya kulingana na kura 173 ambazo hupigwa na waandishi wa habari kutoka duniani kote.