Mchezaji wa Manchester United Paul Pogba amekerwa sana na taarifa ambazo yeye anadai kuwa ni za Upotoshaji ambazo zinaelezea juu ya tabia yake kipindi akiwa na Juventus kabla ya Kwenda Manchester United.
Kiungo huyo ambaye aliutumia muda wake wa miaka 4 akikipiga pale Turin na kuiwezesha Juventus kubeba Mataji ya Seria A kwenye kila msimu kabla ya kurudi tena Old Trafford kwa ada ambayo ilivunja rekodi ya Usajili.
Ilikuwa inasemekana kwamba wakati akiondoka Juventus kwenda Manchester United alidai kuwa "Kama anakwenda mapumzikoni Man U na baadaye atarudi"
Hata hivyo Pogba kwa upande wake anadai kwamba yeye hajawahi kuongea kitu kama hicho.
Pogba anasema yeye alirudi Manchester
United sababu ni klabu ambayo amekulia na alikuwa anajisikia anarudi nyumbani kwake.