Mchezaji wa Real Madrid ameendelea kujitengenezea rekodi yake mpya kwenye Mchezo wa Soka.
Alhamisi hii Mchezaji huyo alifanikiwa kufikisha goli lake la 500 kati ya Mechi 638 wakati Real Madrid ikipata ushindi wa Magoli 2_0 dhidi ya Club America ya Mexico katika mchezo wake wa nusu fainal ya kombe la vilabu bingwa vya dunia huko Nchini Japan.
Magoli hayo yote ni yale aliyofunga akiwa na timu za vilabu pekee ikiwemo Sporting Lisbon ya Ureno aliifungia magoli 5 katika michezo 31.Manchester
United aliifungia magoli 118 kati ya mechi 292 na timu yake ya Real Madrid kashafunga magoli 377 katika Michezo 366 aliyocheza.
Wakati huo huo Ronaldo ndio Mfungaji bora wa muda wote kwenye timu ya Taifa ya Ureno akiwa ameshafunga jumla ya Magoli 68 mpaka sasa.