BREAKING : Mkulima Achomwa Mkuki Mdomoni. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

BREAKING : Mkulima Achomwa Mkuki Mdomoni.

Mkulima mmoja wa kitongoji cha Upwapwani kijiji cha Dodoma Isanga kati ya Masanze jimbo la Mikumi Morogoro amejeruhiwa vibaya kwa kuchomwa mkuki mdomoni na kutokezea nyuma ya Shingo yake.


Ambapo alipelekwa hospitali ya wilayani Kilosa na baadaye akakimbizwa Hospitali ya Mkoa Morogoro ili kufanyiwa Operesheni ya kuondoa Mkuki
huo na kwa matibabu zaidi.

Kijana huyo aliyetambulika kwa Jina la Augustino Mtitu alishambuliwa na wafugaji wa kimasai alipokuwa akimsaidia Jirani yake kufukuza Ng'ombe wasiharibu mazao shambani kwake.katika vurugu hizo inasemekana Mwenyekiti wa kijiji na Mwenyekiti wa kitongohi hicho nao wamejeruhiwa .

Kufuatia tukio hilo Ofisi ya Mbunge wa Mikumi Professor Jay imetoa wito kwa Serikali kuwabaini watu wote waliofanya kitendo hicho cha kinyama na kuhakikisha wanachukuliwa hatua Kali za Kisheria ili kuweza kukomesha vitendo hivi vya kujichukulia Sheria Mkononi inayopelekea kuongezeka kwa uvunjifu Mkubwa wa Amani na Migogoro
Isiyokwisha kati ya Wakulima na Wafugaji wilayani Kilosa.


SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More