Hayawi hayawi na sasa yamekuwa hatimaye staa wa Bongo Flava Diamond Platnumz SIMBA na mpenzi wake Zarinah Hassan Zari the boss lady wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume Prince wa familia aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu kubwa katika familia hiyo.
Mtoto huyo amezaliwa saa 10 na dakika 35 alfajiri kwa saa za Afrika mashariki Jumanne disemba 6 katika hospitali ya NETCARE ya Pretoria Afrika kusini. Diamond na mama yake walisafiri kwenda Afrika kusini kwa ajili ya kumpeleka Zari Hospitali.
Kupitia mtandao wa Instagram Diamond Platnumz ameandika "tarehe 06/12/2016 saa 10 na dakika 35 staa mpya wa kiume alizaliwa katika hospitali ya NETCARE iliyopo mjini Pretoria Afrika kusini kutokana na wazazi wake kutoafikiana muafaka wa mtoto aitwe jina gani,lilipelekea mtoto huyo kuchelewa kupostiwa kwenye mitandao ya kijamii ya wazazi wake.......tusubiri tuone wataishia kumpa jina gani mtoto wao......alimalizia Diamond.Hizi hapa picha za kuzaliwa kwa Prince: