FUNDI PANCHA ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA MISOKOTO 601 YA BANGI. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

FUNDI PANCHA ATUPWA JELA MIAKA 30 KWA KUKUTWA NA MISOKOTO 601 YA BANGI.

Fundi wa kuziba Pancha Harson Solomoni 38 amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kupatikana na Misokoto 601 ya bangi.Bwana Solomoni ni miongoni mwa washitakiwa wa mwanzo  kufungwa kwa sheria hiyo mpya ya udhibiti wa dawa za kulevya iliyosainiwa mei 2015.

Awali sheria ilikuwa inatoa mwanya wa faini kwa mtuhumiwa.Kifungo cha 11(1) cha sheria mpya kinaeleza wazi mtu anayezalisha, kumiliki, kuuza ,kununua au kusafirisha dawa za kulevya ikiwemo Bangi adhabu yake ya chini ni kifungo cha miaka 30 jela.Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Joachim Tiganga baada ya kuridhishwa bila kuacha shaka na ushahidi upande wa Mashitaka.

Wakili wa Serikali Ignas Mwinuka alidai kortini kuwa disemba 1 mwaka 2015 katika maeneo ya Mwika Kimangala Moshi vijijini mshitakiwa alipatikana na kiasi hicho cha bangi pia anadaiwa kuruhusu eneo lake kutumika kuuza Bangi na Gongo.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Tiganga alisema matumizi ya dawa za kulevya yanazidi kuongezeka nchini na kuathiri jamii.

Hivyo mahakama inatoa adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine.
Katika kipindi chote tangu afikishwe kortini kwa mara ya kwanza disemba 1 mwaka jana mshitakiwa alikana mashitaka hadi alipotiwa hatiani na kuhukumiwa jana.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More