Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amepitishwa na chama chake cha Zanu_PF kuwa mgombea Urais katika uchaguzi wa nchi hiyo utakaofanyika mwaka 2018.
Wajumbe wa Zanu_PF walifikia uamuzi huo wa kumpa nafasi nyingine Mugabe mwenye umri wa miaka 92 kupitia mkutano wao uliofanyika katika mji wa kusini mashariki wa Masvingo.
Mugabe amelitawala Taifa hilo tangu lilipopata Uhuru mwaka 1980 lakini bado
Chama chake kinaonesha kuwa na Imani
naye huku kikieleza kuwa anafaa kuwa Rais kwa maisha yake yote.
Wafuasi wake waliimba tongai, tongai, tongai baba wakimaanisha endelea kuongoza baba. Hata hivyo kumekuwa na Maandamano mwaka huu dhidi ya Uongozi wa Kiongozi huyo Pamoja na hali mbaya ya Kiuchumi inayokumba Taifa hilo.
Chama cha Zanu_PF pia kimekabiliwa na
Makabiliano ya wenyewe kwa wenyewe huku makundi hasimu yakipigania kumrithi Rais Mugabe wakati atakapoondoka Madarakani.