Askari wa kikosi cha Suma JKT Moses Mwita amefariki dunia baada ya kujipiga risasi sehemu ya kifuani.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea saa 4:15 asubuhi katika kituo cha mafuta cha BMC mlimani kilichopo mtaa wa Bugando.
Askari huyo alijiua kwa kutumia silaha aina ya Shortgun.Kamanda Msangi alisema taarifa za awali zilibaini kuwa askari huyo alionekana
akizungumza na simu kwa muda mrefu kana kwamba kulikuwa na tatizo lililokuwa linamtatiza.
Na baada ya muda alizunguka nyuma ya kituo na kujipiga risasi Kifuani hivyo kusababisha kifo chake alimalizia kamanda Msangi.