Mkali wa bongo Flava Diamond Platnumz "SIMBA" amempa sifa zake msanii na producer wa Sharobaro Records Bob Junior kama ndiye aliyemfungulia njia ya mafanikio kimuziki.Akizungumza kwenye kipindi cha Ngaz kwa Ngaz Diamond alisema "kiukweli Bob Junior ana mchango mkubwa sana katika maisha yangu kwa sababu ukiangalia nyimbo zangu zote zilizonitoa ni yeye ndiye alikuwa ametengeneza.
"Japokuwa hata kipindi ambacho nilikuwa nazitengeneza inawezekana watu walikuwa hawajamuona kuwa producer mzuri sana lakini Mimi nilikuwa naona mbona huyu natoka naye,nakufa naye,Mimi yaani huyu natoa nyimbo nae na Inahit"alisema Diamond.Akaongeza kwa kusema "nakumbuka tulifanya nyimbo kama sita nenda Kamwambie,Binadamu,Nitarejea,nyimbo kama Mbagala na nyingine tofauti tofauti
"Kila nyimbo alikuwa akinitengenezea akinipa beat nikifika nyumbani naandika vibaya sana".Mpaka nakumbuka ilifika time niliwekewa kama chuki fulani kwa wasanii waliopo pale wakaona mbona unampendelea mtu Fulani yeye akasema Mimi ni Producer natengeneza beat nikimpa msanii kaandikie kitu kikali nikimpa Diamond analeta ngoma Kali".
Kwa upande mwingine Diamond alisema Mbagala ni moja ya nyimbo anazozipenda kwa kuwa aliandika kwa ufanisi Mkubwa.