Mahakama kuu ya Arusha imemnyima dhamana Mbunge wa Arusha Mjini Chadema Godbless Lema.Mahakama hiyo imeeleza kuwa mawakili wa mtuhumiwa huyo walipaswa kuonesha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku 10 kabla ya kukata rufaa.
Hii ni Mara ya 5 Mbunge huyo anakosa dhamana mahakamani tangu alipokamatwa November 3 mwaka huu akiwa mjini Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha katika kesi ya Uchochezi inayomkabili.Katika kesi ya Msingi Lema anatuhumiwa kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya Rais Magufuli kwa madai kuwa mungu ndiye aliyemwambia maneno hayo wakati akiwa anaomba.