Trump aendelea kufanya uteuzi amteua Jeneral James Mattis kuwa waziri wa Ulinzi. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Trump aendelea kufanya uteuzi amteua Jeneral James Mattis kuwa waziri wa Ulinzi.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amefanya mkutano wa kwanza wa hadhara tangu kushinda Urais ambapo amemtangaza Jeneral mstaafu James Mattis kuwa waziri mpya wa Ulinzi.Jeneral Mattis maarufu kama "MAD DOG"ni mwanajeshi wa zamani aliye na sifa ya kuweka mikakati kuwa na msimamo mkali na mpinzani mkubwa wa Iran.

Trump alimfananisha James Mattis na Jeneral George Patton kamanda wa jeshi la Marekani kwenye vita vikuu vya pili ambapo wenzake walimpa jina la "Old Blood and Guts" kutokana na ujasiri wake.Akihutubia mkutano wa hadhara katika jimbo la Ohio Trump ameapa kutumia mamlaka yake kukandamiza kabisa na Ugaidi Marekani.Amesema watu wasiojulikana wanaingia Marekani kutoka Mashariki ya kati na kusema atawazima kabisa.

Rais huyo Mteule amesisitiza kauli yake kwenye kampeni ya kuweka maslahi ya Marekani mbele akisema Raia wa Marekani wanajali zaidi masuala ya ndani ya nchi na siyo matukio ya kimataifa. Aidha amelaani lugha ya uchochezi na mgawanyiko.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More