Baada ya takribani miaka kadhaa ya Uadui mkubwa kati ya Msanii Lady Jaydee na Clouds Media Group msanii Huyo ametangaza kuwa hana tatizo tena na Clouds.Uamuzi huo umekuja baada ya Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba kusema kuwa wapo tayari kuanza kucheza nyimbo za muimbaji huyo iwapo atawapa ruhusa.
Lady jaydee akijibu ofa hiyo amesikika akisema kwenye interview yake "nimesikia kauli ya Ruge kwa namna alivyoiongea na nafasi aliyokuwa nayo,
sioni kama kuna kitu kibaya chochote
Alichokifanya kwa jinsi ambavyo amezungumza naona amejibu sahihi tu"alisema "hajanipigia simu wala sijampigia simu,kwa hiyo sio kwamba tumeongea kitu chochote lakini nayaona
tu ni maamuzi makubwa ambayo yamefanyika hapo,hatujaongea kwa sababu tulikuwa na mgogoro".
Ameongeza kuwa kama kuna kauli yoyote itatakiwa kutoka Management itatoa kauli hiyo ya nini kitafuata alimalizia Lady jaydee.
Sasa kupitia kipindi cha Amplifaya cha Clouds fm Uongozi wa Lady Jaydee ulitoa taarifa yake rasmi kuhusiana na kuwa tayari kufanya kazi tena na kituo hicho namnukuu "Hatuna tatizo na Clouds Media Group kuanza kupiga nyimbo za Lady Jaydee wanaweza kupiga wakati wowote watakapokuwa tayari kwakuwa Chochote kilichotokea
Hapo nyuma kimefikia tamati la msingi sasa ni Amani na Upendo vitawale".
Yalisema maelezo hayo "Kuanzia Leo wana Uhuru Clouds kupiga na kutaja jina
La Lady Jaydee kadri wawezavyo".
Ilimalizia kauli hiyo.