Maneno ya Mtoto wa Godbless Lema baada ya Baba yake Kurudishwa Rumande. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Maneno ya Mtoto wa Godbless Lema baada ya Baba yake Kurudishwa Rumande.

December 2 kwa Mara ya 5 mbunge wa Arusha Mjini Chadema Godbless Lema alikosa dhamana katika mahakama kuu kanda ya Arusha na hivyo kulazimishwa kurudi rumande.

Mbunge huyo alikamatwa Nov 3 mwaka huu akiwa katika vikao vya bunge mjini Dodoma akituhumiwa kutenda kosa la Uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli.

Lema alidai kuwa yeye ni mwombaji na alipokuwa akiomba Mungu alimuonesha kuwa Rais Magufuli asipojirekebisha atakufa.Wakati Lema akirejeshwa rumande mke wake na watoto wake walikuwa mahakamani hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari mtoto wa kwanza wa Mbunge huyo Allbless Lema alisema "Yeye haoni shida baba yake kuendelea kukaa rumande sababu anapigania haki ya familia yake na watanzania wote".Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena February 2 2017.

Mke wa Godbless Lema akiwa na watoto
wake.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More