Breaking :Mganga auawa kwa kutaka kubaka Mteja. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking :Mganga auawa kwa kutaka kubaka Mteja.

Mganga wa Kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje 55 mkazi wa Kijiji cha Singita kilichopo kata ya Usanda wilayani shinyanga ameuawa kwa kupigwa na Wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 jina linahifadhiwa.

Mwanamke huyo aliyekwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Muliro Muliro tukio hilo lilitokea November 29 mwaka huu akisema lilitokea majira ya saa 5 asubuhi.Alisema kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa hospital baada ya kujeruhiwa kwa kiti chenye ncha Kali katika jicho la kulia na kupigwa kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukilia sheria mkononi.

"Watu hao walijichukulia sheria mkononi baada ya Mganga huyo kujaribu kumbaka mwanamke mkazi
wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze kupata mtoto" alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni Tamaa za Kimwili na Uongo wa Kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya kumleweshwa kwa dawa za kienyeji lakini alifanikiwa kupiga kelele na ndipo wananchi walipomvamia Mganga huyo .

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More